Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 21Article 552877

Habari Kuu of Saturday, 21 August 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Mapendekezo 7 Tume ya Uchaguzi - Video

Mapendekezo 7 Tume ya Uchaguzi - Video play videoMapendekezo 7 Tume ya Uchaguzi - Video

WADAU wa Uchaguzi na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imependekeza mambo saba kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan likiwemo la kuweka watendaji wa Tume hadi ngazi za Halmashauri ili kuongeza ufanisi hasa wakati wa chaguzi.

Mambo mengine ni; 1. Kutungwa kwa sheria ya uchaguzi ambayo itaiwezesha tume kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi zaidi 2. Mamlaka husika ziangalie uwezekano wa kuunganisha Sheria ya Taifa ya uchaguzi na Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili kurahisisha utekelezaji wa sheria hizo. 3. Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Serikalu Kuu usimamiwe na Mamlaka moja 4. Sheria za uchaguzi zitafsiliwe kwa lugha ya Kishwahili 5. Serikali inangalie uwezekano wa kuwezesha kifedha asasi na taasisi zinazotoa elimu ya mpiga kura katika nafasi mbalimbali za uchaguzi. 6. Wagombea ubunge na udiwani wanaopita pila kupingwa wapigiwe kura.