Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 12Article 551218

Uhalifu & Adhabu of Thursday, 12 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Mapenzi yameua watu 91 ndani ya miezi sita

Msemaji wa Polisi, David Misime Msemaji wa Polisi, David Misime

Watu 222 wamefariki dunia katika kipindi cha January hadi July Mwaka huu nchini Tanzania kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo wivu wa kimapenzi, Ugoni na Wizi.

Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini David Misime, ametoa mfano wa matukia yakikatili likiwemo tukio la fumanizi na kusabisha kuvuja kwa picha mbaya mitandano lilitokea tarehe 29july kongowe Mbagala jijini Dar es salaam.

pamoja na tukio la kinyama lilitokea wilaya ya korogwe katika jiji cha shemsi ambapo kijana mmoja ambaye alikuwa anatuhumiwa na wizi wa kuaminiwa aliazima pikipiki kwa mtu akakawia kuirejesha nakupelekea kukatwa mapanga na watu hao kisha kuburuzwa kwenye gari mpaka kupelekea Umauti wake.

Akizungumza na wanahabri Jijini Arusha David amesema, kati ya vifo hivyo 91 ni ya mauaji kutokana na wivu wa mapenzi na ugoni, wizi ni 98 na mengine yakiwa ni pamoja na kuwachoma moto watoto kwa tuhuma za kuiba fedha.