Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 07Article 541492

Habari Kuu of Monday, 7 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Marufuku kufukuza watoto hawa shuleni- Waziri Elimu

Marufuku kufukuza watoto hawa shuleni- Waziri Elimu Marufuku kufukuza watoto hawa shuleni- Waziri Elimu

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amepiga marufuku wanafunzi kufukuzwa shule sababu ya wazazi wao kutochangia maendeleo ya shule.

Waziri Ndalichako ametoa majibu hayo Bungeni Dodoma leo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Aida Kenani (Chadema).

Kenani alitaka kujua, serikali inatoa kauli gani kuhusu elimu bila ada au ni elimu bila malipo kwani wananchi wamekuwa wakikataa kushiriki katika shughuli za kuchangia maendeleo kutokana na kudhani elimu hiyo inatolewa bure.

Profesa Ndalichako alisema, waraka namba 3 wa mwaka 2016 unaeleza wazi kwamba wazazi wana wajibu wa kuchangia maendeleo wakishirikiana na serikali.

Profesa Ndalichako alisema kwa kuchangia maendeleo, kunakuwa na mazingira bora ya wanafunzi kupata elimu bora, lakini wanafunzi hao wasifukuzwe kwa sababu ya wazazi wao kutoshiriki katika maendeleo ya shule.