Uko hapa: NyumbaniHabari2021 10 22Article 564901

Habari Kuu of Friday, 22 October 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

"Marufuku kulipana posho kwa fedha za IMF" - Waziri Mkuu

"Marufuku kulipana posho kwa fedha za IMF" - Waziri Mkuu

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Wakuu wa Mikoa yote nchi kusimamia kwa karibu fedha maalum sh trilioni 1.3 zilizotolewa na Shirila la Fedha la Kimataifa (IMF) ili kuimarisha huduma za jamii.

Majaliwa ameyasema hayo leo alipokutana na Kamati ya Kitaifa inayosimia miradi ya fedha za kuimarisha huduma za kijamii.

“Kule mikoani kutakuwa na Kamati maalum na Mkuu wa Mkoa ndiye atakuwa Mwenyekiti na Katibu Tawala atakuwa katibu wao.”amesema na kuongeza

“Pia kutakuwa na mchumi, Mhandisi wa Mkoa, Afisa Manunuzi, Afisa Elimu, Mganga Mkuu wa Mkoa, Mwanasheria, Mratibu wa Sekta na tumemuongeza Mhandisi wa TARURA, kwani atahitajika japo hayumo kwenye sekretarieti ya mkoa.” amesema

Majaliwa, amesema Wenyeviti wa Kamati ya ulinzi ya mkoa (KUU) watakuwa na jukumu la kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi hiyo na kama kutakuwa na suala la rushwa wataingia na kuchukua hatua.

“Katika kipindi cha miezi tisa, tunatakiwa tuwe tumekamilisha miradi yote,” amesema.

Amesema timu hiyo nido itawajibika kwenda maeneo ya vijijini kuona kama kazi inafanyika kwa viwango vinavyotakiwa kwani kuna baadhi ya miradi utekelezaji wake unapaswa uwe umekamilika ndani ya miezi mitatu.

Aidha Majaliwa ametaka vifaa vitakavyotumika kwenye miradi hiyo kutumia ledger.

“Manunuzi haya si ya kutoa fedha mfukoni yakaishia hapo, ni lazima kuwe na ledger, nimebaini kwenye miradi mingi BOQ zinaandaliwa lakini kwenye manunuzi bei inakuwa tofauti na miradi inakwama kukamilika.

Aidha kuhusu posho, amesema “Hakuna mtu yeyote anayepaswa kudai posho katika kazi hii, tukifanya hivyo hii miradi haitakamilika, hata sisi hapa kwenye kamati hii Mheshimiwa Rais hajatoa posho, san asana ametuongezea majukumu,”amesema

Awali, akiwasilisha mchanganuo wa fedha hizo za IMF Sh trilioni 1.3, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba, alisema Elimu imepangiwa sh bilioni 139.4, Afya sh bilioni 446.9, utalii sh bilioni 90.2, Zanzibar sh bilioni 231, Tasaf sh bilioi 5.5, vijana, wanawake na wenye ulemavu sh bilioni 5 na uratibu sh bilioni 5.