Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 18Article 552109

Habari Kuu of Wednesday, 18 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Masharti mapya kuingia Bungeni Dodoma

Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Uongozi wa Bunge la Tanzania, umeweka utaratibu mpya wa uendeshaji wa vikako vya kamati utakao dhibiti mikusanyiko kwa kuzingatia Marufuku zinazotolewa na Wizara ya afya nchini za kujikinga na ugonjwa wa Corona.

Hatua hii imefikiwa wakati Bunge likijiandaa na mikutano ya Kamati 14 za kudumu, ambayo hukusanya Wabunge, waandishi wa Habari, Watendaji wa Serikali na wageni mbali mbali.

Katika kutekeleza kwa vitendo tahadhari za kiafya zinazotolewa na Serikali, Uongozi wa Bunge umeweka utaratibu wa uendeshaji wa Vikao vya Kamati kwa kuvigawa kwa kufuata tofauti ya muda wa kukusanyika, huku idadi ya watendaji wanaoongozana na Mawaziri haipaswi kuzidi Maafisa watano kwa kila Wizara.

Aidha, Wageni watakaoruhusiwa Bungeni kwa kipindi hiki ni Wageni wanaofika Ofisini kwa shughuli za kiofisi, Waandishi wa Habari waliosajiliwa kwa ajili ya kutoa habari za Kibunge pamoja na Wadau watakaohudhuria Vikao vya Kamati kwa ajili ya kutoa maoni ambao wataelekezwa na Kamati inayohusika kabla ya Kikao cha kupokea maoni.