Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 24Article 559549

Habari za Afya of Friday, 24 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Masharti ya chanjo Uingereza yazua migogoro

Chanjo Chanjo

Serikali nchini Uingereza imezua mgogoro kufuatia hatua yake ya kutoruhusu watu kuingia nchini humo waliochoma chanjo tofauti na ile ambayo serikali ya nchi hiyo imezipendekeza.

Serikali ya Uingerza ilizipendekeza Chanjo za Pfizer na Mordena kutumika kwa raia wake.

Katika kupambana na Maambukizi ya Corona Serikali ya Uingereza ilipiga marufuku baadhi ya nchi hususani zilizpo katika mstari mwekundu kuingia nchini Uingereza.

Siku za karibuni waliondoa baadhi ya nchi zilizokua zimefungiwa kuingia nchini humo kutokana na idadi ya maambukizi kuwa kubwa katika nchi hizo lakini walitakiwa kwanza kujitenga kwa siku zisizopungua 10.

Chanjo aina ya Atrazenace inayozalishwa nchini India imekuwa ikinunuliwa na kutolewa katika mataifa mbalimbali kupitia mradi wa COVAX unaosaidia nchi zenye uhitaji, na mataifa yaliyo mengi yamechoma chanjo hiyo, Lakini ni miongoni mwa chanjo ambayo haitatambuliwa na Uingereza.

Dr Richard Mihigo, kutoka shirika la Afya Duniani ukanda wa Afrika, amesema mataifa yote wanaakiwa kupata mtandao ambao utatumika kwenye utoaji wa cheti cha chanjo kitachoweza kutumika kila sehemu.

Uingereza imesema wale wote waliopata Chanjo nje ya Uingereza, Umoja wa Ulaya na Marekani wnatakiwa kujitenga pindi wanapoingia Uingereza.