Uko hapa: NyumbaniHabari2021 10 11Article 562468

Habari Kuu of Monday, 11 October 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Masharti ya matumizi ya fedha za IMF

Masharti ya matumizi ya fedha za IMF Masharti ya matumizi ya fedha za IMF

RAIS Samia Suluhu Hassan ametoa masharti mazito kwa mawaziri na wakurugenzi wa halmashauri pamoja na timu zao akitahadharisha kuwa hatakuwa na huruma na mtu katika matumizi ya fedha za Shirika la Fedha Duniani IMF.

"Kwenye fedha hii sina huruma na Mtu kwasababu nina uwezo wa kupata mikopo mingine nafuu tukivurunda hapa tutajitia doa, sitokuwa na huruma na Mtu kuanzia Mawaziri wangu mpaka chini kwa Wakurugenzi," amesema wakati wa kuzindua kampeni ya maendeleo na mapambano dhidi ya UVIKO-19 jijini Dodoma.

Tanzania imepokea zaidi ya Sh trilioni 1.3 kutoka Shirika la Fedha Duniani kama mkopo wa masharti nafuu kukabiliana na athari za janga la Korona.

Rais Samia amesema fedha hizo za mkopo zinaenda kuleta mabadiliko makubwa nchini kote nakusisitiza haja ya kufafanua matumizi ya mkopo huo nafuu ambao amedai utalipwa na wananchi. “Kwa sababu hiyo ni lazima mjue umekwenda wapi. Tukidumisha Amani, usalama na utulivu, miradi itafanyika haraka na wananchi watafaidika.”

Kwa mujibu wa taarifa ya Waziri wa Fedha na Mipango Dk Mwigulu Nchemba matumizi ya fedha hizo ni pamoja na Kujenga madarasa mapya 15,000 ya sekondari, Kujenga madarasa 3,000 shule za msingi shikizi na Kutengeneza madawati 462,795.

Fedha hizo zitatumika Kumalizia ujenzi wa vyuo vya VETA 32, kununua Magari 25 ya kuchimba visima vya maji, kununua Mitambo 5 ya kujenga mabwawa ya maji na Kujenga ICU 72. Amesema pia zitatumika kununua Magari ya wagongwa (Ambulance) 395 na ya chanjo 214, kuweka Mifumo ya Oxygen hospitali 82 na kununua Mitungi ya gesi 4,640.

Waziri Mwigulu amesema fedha hizo zitanunua Mitambo ya kuzalisha hewa ya Oksijeni 40, kununua Vitanda vya wagonjwa 2,700, X-ray za kisasa 85, CT- Scan 29 na mashine za MRI kwa hospitali zote za kanda.