Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 27Article 559855

Habari Kuu of Monday, 27 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

"Masoko yaliyo tupu yageuzwe kumbi za harusi"- Rais Samia

Rais Samia azitaka Halmashauri kuwashirikisha wananchi ujenzi wa masoko. Rais Samia azitaka Halmashauri kuwashirikisha wananchi ujenzi wa masoko.

Rais Samia, amepinga vitendo vya Halmashauri kujenga masoko mbali na makazi ya watu hali inayopelekea wananchi kushindwa kufika katika masoko hayo na kuisababishia hasara Serikali.

Ametoa kauli hii wakati akifungua Mkutano Maalum wa uchaguzi wa viongozi wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania-ALAT, unaofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center jijini Dodoma, leo tarehe 27 Septemba, 2021.

Rais Samia, amesema kuwa vitendo hivyo ni vya ubadhilifu wa fedha, huku akiwataka viongozi wote wa Halmashaurizote nchini kuwashirikisha wananchi kwenye mambo yanayo wagusa moja kwa kwa moja.

Amelitolea mfano soko jipya la Temeke lilipo jijini Dar es Salaam, ambalo limejengwa mbali na makazi ya watu hivyo kupelekea Halmashauri kutangaza baadhi ya ofa kama michezo ya watoto ili kuweza kuwavuta watu kufika sokoni hapo.

"Kabla ya kujenga masoko, kuna kitu kinaitwa feasibility study, kingefanyika vizuri soko lisingekwenda kujengwa huko.., kuna masoko mengi yamejengwa matupu, naona halmashauri wakageuze tu ma-hall ya harusi, ili yaingize fedha, lakini sio maeneo ya wajasiriamali".Rais Samia.