Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 08Article 584158

Habari Kuu of Saturday, 8 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Mavunde Acharuka: Juni Umeme Uwashwe

Mavunde Acharuka: Juni Umeme Uwashwe Mavunde Acharuka: Juni Umeme Uwashwe

MBUNGE wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde ameridhishwa na kasi ya usimikaji nguzo katika Kata hiyo na kumtaka Mkandarasi kukamilisha maeneo yaliyobaki ya Mtaa wa Makulu na Mwegamile ili ifikapo Juni,2022 eneo lote liwe limewashwa umeme.

Mavunde ameyasema hayo alipotembelea mradi huo akiambatana na diwani wa kata ya Mbalawala Charles Ngh'ambi katika kukagua mradi huo unaotekelezwa na Kampuni ya Umeme ya Ceylex chini ya mradi wa PERI URBAN.

Aidha akishukuru kwa niaba ya wananchi, diwani wa kata ya Mbalawala Charles Ngh'ambi ameishukuru serikali chini ya Rais Samia Suluhu, kwa kasi ya utekelezaji wa mradi huo wa umeme na kuahidi kushirikiana na mkandarasi ili kazi ya usambazaji umeme ikamilike mapema na wananchi waweza kutumia nishati hiyo kwa matumizi ya kiuchumi na kijamii.