Uko hapa: NyumbaniHabari2021 05 28Article 540346

Habari Kuu ya

Chanzo: millardayo.com

Mazungumzo ya Rais Samia na Msaidizi wa Katibu Mkuu UN

Mazungumzo ya Rais Samia na Msaidizi wa Katibu Mkuu UN Mazungumzo ya Rais Samia na Msaidizi wa Katibu Mkuu UN

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Wanawake (UN-Women) Dkt. Phumzile Mlambo-Ngcuka kuhusu kuendeleza agenda zinazowahusu wanawake.

Dkt. Phumzile amemshukuru Rais Samia kwa namna anavyounga mkono juhudi za kupigania masuala ya wanawake na ameahidi kuwa UN-Women itamuunga mkono katika juhudi hizo.

Amemualika kushiriki katika mkutano utakaojadilia masuala ya kijinsia uliopangwa kufanyika tarehe 30th Juni, 2021 huko Paris, Ufaransa ambao madhumuni yake ni kuchagiza usawa wa kijinsia kama yalivyokubaliwa katika mkutano wa Beijing uliofanyika mwaka 1995 baada ya kuonekana baadhi ya maazimio yanasuasua.

Kuelekea mkutano huo nchi zitakazoshiriki zimegawanywa katika maeneo 6 ya kufanyia kazi na Rais Samia amekubali kuwa kiongozi katika eneo la haki za kiuchumi.

Aidha, Dkt. Phumzile ameeleza kufurahishwa kwake na sekta binafsi ya Tanzania ambayo imekubali kushirikiana na Serikali kusaidia juhudi za kuleta usawa wa kijinsia katika masuala ya kiuchumi kwa wanawake.

Kwa upande wake, Rais Samia ameipongeza UN-Women kwa juhudi kubwa za kupigania masuala ya wanawake ikiwemo maazimio ya Beijing na ameeleza kuwa Tanzania ipo tayari kuungana na UN-Women katika kuongeza msukumo wa utekelezaji wake.Amebainisha kuwa japo Tanzania bado haijafikia kiwango cha usawa wa kijinsia cha 50/50 katika uongozi, katika kipindi chake atahakikisha anaongeza jitihada za kufikia usawa huo.

Rais Samia ameishukuru UN-Women kwa utayari wake wa kuisaidia Tanzania katika kukabiliana na janga la ugonjwa wa Korona (Covid-19).

TAZAMA MSAFARA WA MWANA WA KIFALME ULIVYOINGIA IKULU AKIKUTANA NA RAIS SAMIA

Join our Newsletter