Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 03Article 540895

xxxxxxxxxxx of Thursday, 3 June 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Mbaroni Kisutu Kwa Tuhuma za Kusafirisha Dawa za Kulevya

Mbaroni Kisutu Kwa Tuhuma za Kusafirisha Dawa za Kulevya June 3, 2021 by Denis MtimaWatu watatu akiwemo Afisa Utawala wa kampuni ya ujenzi ya Makame Mwinyi Generals Supplies, Batuli Bakari (39) na fundi umeme Said Abdallah (33), wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka la kusafirisha dawa za kulevya.

Wakili wa serikali Yusuph Abood akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Rita Tarimo amedai kuwa Mei 5, 2021 huko Mikocheni katika manispaa y Kinondoni jijini Dar es s Salaam washtakiwa walikutwa wakisafirisha gramu 194.93 za dawa za kulevya aina ya Heroine Hydrochloride.

Hata hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za dawa za kulevya.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 17, 2021 kwa ajili ya kutajwa na upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika.

Join our Newsletter