Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 30Article 554482

Habari Kuu of Monday, 30 August 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Mbowe Amgeuzia Kibao DPP

Mbowe Amgeuzia Kibao DPP Mbowe Amgeuzia Kibao DPP

Baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam kukubali ombi la Mawakili wa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe la kuhudhuria shauri lake la Kikatiba alilolifungua dhidi ya Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka (DPP), Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) mda huu amefikishwa katika Mahakama kuu kwa ajili ya kusikiliza shauri hilo.

Katika shauri hilo namba 21 la mwaka 2021 linalosikilizwa mbele ya jopo la Majaji watatu John Mgeta, Steven Magoiga na Leila Mgonya lilipangwa kutajwa leo Agosti 30, 2021.

Katika kesi hiyo, Mbowe anapinga hatua ya kushtakiwa kwa kosa la ugaidi kupelekwa mahakamani kimyakimya bila kumtaarifu wakili wake.

Sambamba na madai hayo ya anadai haki zake kukiukwa kwa kutokujulishwa na kupewa fursa ya kuwasilisha kuwajulisha ndugu zake na wakili wake, pia Mbowe anadai kuwa wakati alipokwa ameshikiliwa katika kituo cha Polisi Oysterbay alikuwa akipokea kauli za kejeli na vitisho kutoka kwa afisa wa polisi.

Mbowe alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakikmu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, Julai 26, 2021 na kusomewa mashtaka ya ugaidi katika kesi aliyounganishwa na washtakiwa wengine waliokuwa wameshapandishwa kizimbani tangu mwaka jana 2020.