Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 07Article 541417

Siasa of Monday, 7 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Mbowe: Nipo tayari kuachia madaraka

Mbowe: Nipo tayari kuachia madaraka Mbowe: Nipo tayari kuachia madaraka

CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinatarajia kumchagua mwenyekiti wake kitaifa, Desemba 2023.

Mwenyekiti Chadema, Freeman Mbowe, alisema hayo jana mjini Tabora wakati akizugumza na wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chadema, Kanda ya Magharibi.

Mbowe alisema chama hicho licha ya changamoto kadhaa, bado kiko imara na kimeendelea kuungwa mkono na wananchi hasa vijana.

Aliwapongeza watangulizi wake akiwemo muasisi wake, Edwin Mtei, kwa kukijengea msingi imara na kubainisha kuwa, amekitumikia kwa muda mrefu na sasa kina watu makini wenye maono mapya wanaoweza kukiongoza kwa mafanikio makubwa.

“Natangaza kuwa mwaka 2023 utakuwa mwaka wa uchaguzi mkuu wa chama chetu katika ngazi zote kuanzia ngazi ya shina, tawi, wilaya, mkoa hadi taifa kwa nchi nzima na mwenyekiti wa taifa atachaguliwa mwezi Desemba 2023,” alisema.

Mbowe alisema Chadema kina wanachama wasomi na uwezo mkubwa, hivyo yeyote anayetaka kugombea kuanzia sasa ajiandae na kwamba yuko tayari kuachia madaraka ya kukiongoza.

Alisema dhamira ya Chadema kushika dola ipo pale pale na milango iko wazi kwa mtu yeyote anayetaka kujiunga na chama hicho ili kuongeza nguvu.

“Sina tatizo na mtu yeyote mwenye maono mapya ya kimaendeleo atakayejitokeza kunirithi, tunataka damu mpya, niko tayari kumpa ushirikiano, tunataka kukijenga upya kwa kasi ya ajabu na kukifanya kuwa cha kidigitali zaidi,” alisema.

Alisema wanataka chama hicho kianze kuendeshwa kidigiti zaidi na kwamba usajili wa wanachama nchi nzima utafanyika upya na hata ada zitalipwa kidigiti.

Join our Newsletter