Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 10Article 556645

Uhalifu & Adhabu of Friday, 10 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Mbowe abadilishiwa Jaji kwenye kesi yake

Freeman Aikael Mbowe, Mwenyeketi wa CHADEMA Freeman Aikael Mbowe, Mwenyeketi wa CHADEMA

Kesi ya Uhujumu Uchumi Namba 16/2021 yenye mashtaka ya Ugaidi, inayomkabili mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu, inaendelea kusikilizwa leo Ijumaa Septemba 10, 2021 hapa katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi jijini Dar es Salaam Mbele ya Jaji mwingine, Mustapha Siyani.

Hii ni baada ya Jaji Elinaza Luvanda aliyekuwa akisikiliza kesi hii, kuchukua uamuzi wa kujitoa kutokana Mbowe na wenzake kudai kuwa hatotenda haki wakati wa usikilizwaji wa kesi hiyo.

Awali katika usikilizaji wa kesi hii Mahakama ilipinga mapingamizi yaliyowasilihwa na upande wa Utetezi.