Uko hapa: NyumbaniHabari2021 05 27Article 540091

xxxxxxxxxxx ya

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Mbowe ampongeza Rais Samia

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amempongeza Rais Samia Suluhu kwa kurejesha tabasamu kwa wananchi, huku akiwa tayari kukutana naye kuzungumzia masuala ya siasa.

Aidha, chama hicho leo kinazindua Programu ya Chadema Digitali yenye lengo la kusajili wanachama sanjari na mpango wa baadaye wa kuanzisha Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo (Saccos) pasipo kutegemea mikopo ya benki mbalimbali au taasisi za fedha.

Mbowe alitoa pongezi hizo jana jijini Arusha wakati akizungumza na wanachama na viongozi wa Chadema kutoka wilaya mbalimbali za Mkoa wa Arusha kuhusu uboreshaji wa chama hicho.

Alisema anampongeza Rais Samia kwa kurejesha imani kwa Watanzania waliokata tamaa ambao alidai baadhi yao wameonewa na wengine kubambikiwa kesi.

Join our Newsletter