Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 27Article 559843

Uhalifu & Adhabu of Monday, 27 September 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Mbowe na Wenzake Mahakamani Tena

Mbowe na Wenzake Mahakamani Tena Mbowe na Wenzake Mahakamani Tena

LEO Jumatatu, Septemba 27, 2021, Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mhe. Freeman Mbowe na wenzake watatu wamefiika Katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu uchumi kwa ajili ya kuendelea kusikiliza kesi inayowakabili.

Kesi hiyo namba 16/2021 inayomkabili Mbowe na wenzake watatu ipo hatua ya usikilizwaji wa mashahidi upande wa utetezi katika shauri dogo ya kesi msingi ambapo shahidi namba 1 ambaye ni mtuhumiwa namba 2 Adam Kasekwa anaendelea kutoa ushahidi.

Kesi hiyo ambayo inasikilizwa na Jaji Mustapha Siyan baada ya Jaji Eliezer Luvanda aliyekuwa akiisikiliza hapo awali kujiondoa kutokana na upande wa Utetezi kutokuwa na Imani naye.

Ikumbukwe kuwa Mbowe na wenzake wanakabiliwa na Mashtaka sita likiwemo la Uhujumu uchumi pamoja nala kula njama yakufadhili genge la ugaidi.