Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 23Article 573727

Habari Kuu of Tuesday, 23 November 2021

Chanzo: millardayo.com

Mchumba wa Khashoggi amwandikia barua Justin Bieber

Mchumba wa Khashoggi amwandikia barua Justin Bieber Mchumba wa Khashoggi amwandikia barua Justin Bieber

Mchumba wa aliyekuwa mwandishi wa habari maarufu wa Saudi Arabia, Jamal Khashoggi, amemwandikia barua staa wa muziki wa Pop, Justin Bieber, akimwomba kutokwenda kufanya ‘shoo’ katika taifa hilo la Kiarabu.

Katika ujumbe wake kwa Bieber, Hatice aliyekwishavishwa pete na Khashoggi, amesema: “Usiende kuwaimbia watu waliohusika kumuua mpenzi wangu, Jamal” – aliandika katika barua iliyochapishwa na gazeti la Washington Post.

Bieber anatarajiwa kuingia Saudi mwezi ujao akijumuika na wasanii wengine wakiwemo A$AP Rocky, David Guetta na Jason Derulo lakini bibiye Hatice Cengiz amemtaka kubadili uamuzi ili uwe ni ujumbe dhidi ya Serikali ya nchi hiyo iliyohusika katika kifo cha mpenzi wake, Khashoggi.

Khashoggi aliuawa mwaka 2018 akiwa jijini Istanbul, Uturuki, huku ikielezwa kuwa ulikuwa ni mpango wa Serikali ya Saudi kwa kuwa alikuwa akiikosoa mara kwa mara.