Uko hapa: NyumbaniHabari2021 12 05Article 576322

Habari Kuu of Sunday, 5 December 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Mfahamu Padri Rumisho, Engineer, Meja wa Jeshi, Komando na Muhitimu wa Phd ya Uhandisi Hapa Bongo

Padre Rumisho Padre Rumisho

Padri Henry Rimisho wa kanisa katoliki, jimbo la Moshi leo ametunukiwa shahada ya uzamivu katika usanifu majengo (PhD in Architecture) ya chuo kikuu cha Ardhi. Padri Rimisho ana shahada ya sayansi katika usanifu majengo (Bachelor of Architecture) na Shahada ya umahiri katika usanifu majengo (Master of Architecture) zote kutoka chuo kikuu cha Ardhi.

Baada ya miaka minne ya kusoma kwa bidii, kufanya tafiti na kuandika maandiko mengi ya kutaalamu, hatimaye leo ametunukiwa shahada ya uzamivu katika usanifu majengo (PhD in Architecture). Padri Rimisho ni Professional Architect aliyesajiliwa na Board ya Wasanifu Majengo na wakadiriaji majenzi (AQRB). Amesanifu majengo mengi ndani na nje ya nchi, pamoja na majengo ya jeshi. Pia ni Mhadhiri wa chuo kikuu cha Ardhi.

Kwa upande mwingine Padri Rimisho ni Askari wa jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) mwenye cheo cha Meja (cheo kinachofuata baada ya Kepteni). Pia ni Komandoo wa JWTZ (Millitary Ordinariate) na ameshiriki operesheni kadhaa za kijeshi nje ya nchi, ikiwemo operesheni ya kulinda amani ya Darfur.

Padri Rimisho ni Mmisionari wa shirika la Apostles of Jesus, ambaye ana shahada ya kwanza ya Falsafa (Bacholer degree in Philosophy) na Shahada ya Utaalimungu (Bachelor degree in Theology) kabla ya kubarikiwa kuwa Padri.

Kwahiyo Rimisho ni Padri, ni Meja wa JWTZ, ni Komandoo katika uwanja wa vita, na ni Msanifu mwenye shahada ya uzamivu (PhD) katika usanifu majengo. Kwa hiyo unaweza kumuita Rev.Fr.Dr.Major Henry Rumisho (PhD).

Kama uliwahi kusikia neno "Genius" basi tafsiri halisi ya neno hilo ni Padri Rimisho. Uwe Padri, uwe mwanajeshi, uwe Komandoo, uwe Msanifu majengo, uwe PhD holder, vyote kwa wakati mmoja sio kitu rahisi kabisa. Huu ni utumishi wa aina yake na ni watu wachache walioweza kuexplore karama zao zote kama Padri Rimisho. Hongera Rev.Fr.Dr.Major Henry Rumisho (PhD), Hongera kanisa katoliki, Hongera JWTZ.!