Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 14Article 542629

Uhalifu & Adhabu of Monday, 14 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Mfanyabiashara mbaroni utapeli mtandaoni

Mfanyabiashara mbaroni utapeli mtandaoni Mfanyabiashara mbaroni utapeli mtandaoni

JESHI la Polisi Mkoa wa Katavi limemkamata mfanyabiashara, Andrew Aloyce, maarufu kwa jina la Komba (39) akituhumiwa kutapeli kwa kujifanya mkandarasi na mtathimini wa majengo.

Kijana huyo mkazi wa Bahari Beach, Dar es Salaam, anatuhumiwa kutapeli wananchi akitumia mitandao ya kijamii.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Benjamin Kuzaga, alisema Aloyce alikamatwa akituhumiwa kutapeli wananch kwa kutumia jina la kampuni ya Amorin Group Of Companies Limited ya Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Kamanda Kuzaga, kijana huyo alikamatwa Juni 12 mwaka huu mjini Mpanda na wanaendelea kumhoji.

Wakati huohuo; Polisi mkoani Katavi wamekamata watu watano wanaotuhumiwa kuvamia gari lililokuwa likiendeshwa na mfanyabiashara Kakosi John (32) na kumpora fedha taslimu na vitu vyote vikiwa na thamani ya Sh 5,198,000.

Kamanda Kuzaga aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni mfanyabiashara Juma Said (25) mkazi wa Kijiji cha Ng'ombe na Ramadhani Habibu (22) mkazi wa Kijiji cha Ibelamafipa.

Wengine ni Beatus Malima (39), Paulo Joseph (36) na Mussa Petro (35) wote ni wakazi wa kijiji cha Ilunde kilichopo katika wilaya ya Mlele.

Alisema tukio hilo lilitokea Juni 03 mwaka huu katika Barabara ya Inyonga - Ilunde kwenye ranchi iliyopo kwenye Kata ya Ilunde wilayani Mlele mkoani hapa.

Kuzaga alisema siku ya tukio mfanyabiasha, Kakosi John, mkazi wa Igombe "B" alikuwa akiendesha gari yenye namba za usajili T. 932 AJB akiwa na abiria watatu ambao ni Anna Edward (49), mkazi wa uzega Inyonga, James Kasembe (18), mkazi wa Tabora na Joseph Silyvesta (47) mkazi wa Majimoto.

"Walivamiwa na kisha kunyang'anywa fedha taslimu pamoja na vitu mbalimbali vyote vikiwa na thamani ya Sh 5,198,000/= na kisha watuhumiwa hao wakatokomea porini," alieleza.