Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 22Article 573394

Habari Kuu of Monday, 22 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Mfanyakazi Muhimbili Afariki Uwanjani Akivuta Kamba

Mfanyakazi Muhimbili Afariki Uwanjani Akivuta Kamba Mfanyakazi Muhimbili Afariki Uwanjani Akivuta Kamba

Mfanyakazi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Ally Lidengi amefariki uwanjani wakati akicheza mchezo wa kuvuta kamba kwenye mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Taaisi za Umma na sekta binafsi (SHIMMUTA) ambayo yanaendelea mjini Morogoro..

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi mkuu hospital ya Taifa Muhimbili Daktari Prakseda Ogweyo amesema tukio hilo limetokea juzi Novemba 20,2021 katika Uwanja wa Jamhuri Morogoro ambapo amesema marahemu huyo baada ya kuvuta kamba alianguka na alikimbizwa Hospitali ya Rufaa Morogoro tayari alikutwa ameshafariki

Amesema kwa sasa mwili wa marehemu unasafrishwa kuelekea hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi wa chanzo cha kifo chake.