Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 29Article 560410

Diasporian News of Wednesday, 29 September 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Mfumuko wa bei kudhibitiwa Zanzibar

Mfumuko wa bei kudhibitiwa Zanzibar Mfumuko wa bei kudhibitiwa Zanzibar

RAIS wa Zanzibar, Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali itaendelea kuchukua hatua za makusudi katika kudhibiti tatizo la mfumuko wa bei ya mafuta na bidhaa mbalimbali ili kuwapunguzia makali wananchi visiwani Zanzibar.

Rais Mwinyi, ameyasema hayo leo Septemba 29, 2021 katika mkutano na viongozi wa dini ya Kikristo Zanzibar.

Mkutano huo umefanyika kwenye ukumbi wa Amani Utengamano Welezo, Mkoa wa Mjini Magharib.

“Hivi karibuni tumetangaza Serikali itatoa ruzuku, kwenye mafuta ili kuzuia kupanda kwa bei. Mafuta yalikuwa yamefikia sh 2461 tumerudisha sasa mpaka sh 2300.

Amesema lengo la kufanya hivyo hivyo upande wa chakula ili wananchi waweze kumudu maisha ya kila siku.

Aidha, Rais ameendelea kutilia mkazo suala la kudumisha amani na mshikamano miongoni mwa jamii za Wazanzibar huku akisema Serikali itaendelea kutoa huduma kwa wananchi wote pasipo kujali dini wala dhehebu kama katiba inavyoelekeza.

Pia ametumia fursa hiyo kuwapongeza na kuwashukuru viongozi wa dini kwa kuendelea kutoa mchango mkubwa kwenye jamii katika huduma mbalimbali za kijamii.