Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 23Article 573775

Habari Kuu of Tuesday, 23 November 2021

Chanzo: millardayo.com

Mgao wa maji uwe wa uwazi, Visima viwe standby" Aweso

Mgao wa maji uwe wa uwazi, Visima viwe standby Mgao wa maji uwe wa uwazi, Visima viwe standby" Aweso

< Siku 15 zimepita tangu Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kutangaza mgao wa maji, Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema hali bado si shwari na kuagiza DAWASA kuendesha mgao kwa uwazi na usawa.

Aweso ametoa kauli hiyo leo alipotembelea mradi wa visima saba wa Kimbiji ambao unatarajiwa kumaliza changamoto ya maji katika wilaya ya Kigamboni.

“Mara ya kwanza mtambo wa Ruvu chini pampu zetu zilikuwa hazifanyi kazi kwa sababu maji yalikuwa chini kabisa, bado hatuko stable, baada ya kufanyika zile operesheni za kuwaondoa wachepusha maji, zimesaidia yale maji kuingia kwenye mkondo wa mto Ruvu na kutupa nguvu kidogo kwa maana zile pampu ziweze kujiendesha ili watu waweze kupata huduma ya maji” Aweso

“Kwahiyo bado nasisitiza hatuko stable ndiyo maana nasisitiza wananchi kile kidogo tunachokizalisha kinatumika vizuri na tunakihifadhi ili tuweze kuvuka salama,”.

“Utaratibu wa ugawaji maji uwe wazi, kama jumatatu wanapata maji Kigamboni basi wapate, kama Jumanne Sinza iwe hivyo, kingine niwaombe DAWASA visima vyote vilivyochimbwa pembezoni na katikati ya mji viwe standby, vijulikane ili tujipange zaidi vituwezeshe kuvuka salama,” Aweso.