Uko hapa: NyumbaniHabari2021 05 30Article 540631

Habari Kuu of Sunday, 30 May 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Mhagama akutana na ujumbe wa Plan International

Mhagama akutana na ujumbe wa Plan International Mhagama akutana na ujumbe wa Plan International

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera,Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye Ulemavu), Jenista Mhagama, amefanya mazungumzo na

viongozi wa Plan International – Tanzania, ofisini kwake jijini Dodoma.

Ujumbe huo umeongozwa na Mkurugenzi Mkazi wa Plan International-Tanzania.

Katika kikao hicho, viongozi hao wa shirika walipata fursa ya kueleza kwa kina mipango yao ya kushirikiana na serikali kwenye shughuli wanazozifanya.

Walisema wanayo miradi wanayotekeleza katika kuchochea maendeleo ya vijana pamoja na kujumuisha

watu wenye ulemavu kwenye shughuli za maendeleo.

Waziri Mhagama aliwahakikishia kuwa serikali ipo tayari kuendelea kushirikiana nao katika mikakati ya maendeleo ya vijana na masuala ya watu wenye ulemavu.

Alisema atawaelekeza wataalamu wa Ofisi hiyo wakutane na wataalamu wa shirika hilo wapange mikakati ya kushirikiana .

Ofisi ya Waziri Mkuu, (Kazi,vijana, Ajira na Watu wenye ulemavu) inaratibu ma-

suala ya vijana na watu wenye ulemavu kwa uhamasishaji wa vijana, malezi na uwezeshaji wa kiuchumi na kijamii, pia inaratibu masuala ya watu wenye ulemavu kwa kutoa utaalamu na huduma kwa watu wenye ulemavu.

Join our Newsletter