Uko hapa: NyumbaniHabari2021 07 05Article 545455

Habari za Mikoani of Monday, 5 July 2021

Chanzo: dar24.com

Mhandisi Mfugale kuzikwa leo

Mhandisi Mfugale kuzikwa leo Mhandisi Mfugale kuzikwa leo

Maziko ya aliyekuwa Mkuu wa TANROADS (WAKALA WA BARABARA TANZANIA), Mhandisi Patrick Mfugale yatafanyika leo Julai 5, 2021 nyumbani kwao kitongoji cha Ihagaa, kijiji cha Ifunda mkoani Iringa, katika makaburi ya familia walipozikwa wazazi wake..

Akizungumza na Gazeti la Nipashe, Mdogo wa marehemu Mhandisi Mfugale, Joshua Mfugale maesema kuwa kaka yake atazikwa kwenye makaburi hayo kwa sababu ni desturi ya familia kuzikwa katika eneo hilo lililotengwa na familia.

“Kimila katika ukoo wetu hata kama ndugu atafariki umbali kiasi gani lazima mwili wake urudi kuzikwa katika udongo wa nyumbani katika makaburi haya, ukoo wote wakinamfugale wamezikwa hapa na inatusaidia kuweka historia kwa wajukuu zetu na vizaizi vijavyo,” Amesema Joshua.

Aidha Familia imeandaa mazingira mazuri kwa wale wote watakaofika kijijini hapo kushiriki mazishi ya Mhandisi Mfugale.

Mfugale alifariki dunia katika Hospitali ya Benjamini Mkapa Dodoma wakati akipatiwa matibabu, hadi umauti unamkuta ameacha historia ya kujenga barabara zenye urefu wa kilometa 36,258 na madaraja 1,400.

Hata hivyo madaraja aliyosimamia na kusanifu ujenzi wake yameingia katika orodha ya miradi 10 bora kwa urefu Barani Afrika, ikiwemo Daraja la John Pombe Magufuli ambalo likikamilika litakuwa namba sita kwa urefu.