Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 22Article 573577

Habari Kuu of Monday, 22 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Miaka minne kutoweka Azory Agwanda, Polisi wasema bado wanafanya uchunguzi

Miaka minne tangu kutoweka Azory Agwanda, Polisi wasema bado wanafanya uchunguzi Miaka minne tangu kutoweka Azory Agwanda, Polisi wasema bado wanafanya uchunguzi

Ni miaka 4 tangu kutoweka kwa mwandishi wa habari wa kujitegemea wa Tanzania Azory Gwanda huku bado hakuna taarifa kuhusu wapi aliko.

Kamati ya CPJ inayojihusisha na kuwalinda wanahabari - imetoa taarifa yake ikilaumu serikali ya Tanzania kwa kushindwa kufanya uchunguzi wa kuaminika kuhusu hatima ya mwandishi huyo ambaye Kabla ya kutoweka kwake, alikuwa akifanya shughuli za uandishi wa habari katika Wilaya ya Kibiti.

Hata hivyo Msemaji wa Jeshi la polisi nchini Tanzania David Misime amesema suala la Azory lilipokelewa na kufuata taratibu zote za kisheria zinazoelekeza jeshi la polisi namna ya kushughulikia watu ambao wameripotiwa kupotea.

‘’Sisi jeshi la polisi huwa hatukati tamaa,huwa tunaendelea na taratibu zetu kila mara kwenye vikao vyetu vya kufanya tathmini,je watu wangapi walipotea wangapi wamepatikana,nini kifanyike’’…anasema Misime.

Anna Pinoni, mke wa mwandishi wa habari, Azory Gwanda aliyepotea katika mazingira ya kutatanisha Novemba 21, 2017 ameiambia BBC kwamba bado ana imani kuwa mume wake atapatikana.