Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 07Article 541498

Habari za Mikoani ya

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Mikopo nje nje kwa vijana wanaojihusisha na Samaki Kawe

Mikopo nje nje kwa vijana wanaojihusisha na Samaki Kawe Mikopo nje nje kwa vijana wanaojihusisha na Samaki Kawe

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amewashauri Vijana wa Jimbo la Kawe mkoani Dar es Salaam kuunda vikundi ili kufaidi fursa mbalimbali za mikopo zinazotolewa na wizara hiyo.

Kauli hiyo ameitoa Bungeni hapa leo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima (CCM) aliyetaka kujua ni lini serikali itaanza kutoa mikopo kwa vijana wengi wanaovua kwa kutumia mitumbwi midogo katika Bahari ya Hindi?

Naibu Waziri Ulega amesema, vijana wa jimbo hilo wanatakiwa kujiunda katika vikundi ili kupata mikopo inayotolewa na wizara hiyo ikiwemo ya kumununua mashine za boti za uvuvi.

"Pia wanaweza kujiunga katika vikundi ili kupata mikopo ya kutengeneza vichanja vya kukaushia samaki pamoja na kukopa mikopo kwa ajili ya kuzalisha barafu ya kuhifadhia samaki na pia kuwauzia vijana wengine," amesema.

Join our Newsletter