Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 10Article 584593

Habari Kuu of Monday, 10 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Mikopo ya Wanafunzi Vyuo Vikuu ndani ya Saa 24

Mikopo ya Wanafunzi Vyuo Vikuu ndani ya Saa 24 Mikopo ya Wanafunzi Vyuo Vikuu ndani ya Saa 24

BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inatarajia kuanza kuwasajili wanafunzi 70,396 wanufaika wa mwaka wa kwanza katika mfumo wa kidigitali wa malipo ya fedha za mikopo ambao utawawezesha kupokea fedha ndani ya saa 24.

Mkurugenzi wa Upangaji na Utoaji Mikopo HESLB, Dk Veronica Nyahende amesema leo jumapili Januari 9, 2022, kuwa usajili huo utajumuisha kuchukuliwa kwa alama za vidole, taarifa za kibenki, picha pamoja na taarifa za usajili wa wanafunzi vyuoni.

Dk Nyahende amefafanua kuwa usajili huo utafanyika katika taasisi za elimu ya juu nchini kuanzia Jumatatu, Januari 10 hadi Februari 3 mwaka huu.

“Mfumo huu unaitwa ‘Digital Disbursement Solution’ maarufu kama DiDiS na tuliuanzisha mwaka 2018 ili kurahisisha fedha kuwafikia wanafunzi kutoka siku 10 hadi saa 24 hivi sasa,” amesema Dk Nyahende.