Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 19Article 552382

Habari za Mikoani of Thursday, 19 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Mikusanyiko Mochwari yapigwa Stop Iringa!

Mirundikano Mochwari yapigwa Stop Mirundikano Mochwari yapigwa Stop

Katika juhudi za kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa UVIKO-19, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Queen Sendiga, amepiga marufuku tabia ya watu kurundikana kwa ajili ya kuchukua miili ya wapendwa wao katika eneo la chumba cha kuhifadhia maiti kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa na badala yake amesema idadi ya watu wanaoruhusiwa kufika katika eneo hilo wasizidi wanne.

Akizungumza mara baada ya kufanya ziara kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa, Mkuu huyo wa mkoa Queen Sendiga amesema katika zama hizi za maradhi ya kuambukiza kama UVIKO-19 si busara kwa watu kujazana ktk chumba cha kuhifadhia maiti na hivyo amemuagiza Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa kuhakikisha kunakuwepo na utaratibu mzuri wa kuruhusu watu kufika eneo hilo na kuchukua miili ya wapendwa wao.

Toka zoezi la utoaji wa hiari wa chanjo ya UVIKO-19 kuzinduliwa, wakazi wa mkoa wa Iringa wameendelea kujitokeza kupata chanjo hiyo kupitia vituo 15 vilivyotengwa mkoa mzima.