Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 18Article 558172

Habari Kuu of Saturday, 18 September 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Miradi ya Tsh. Bilioni 855 kukaguliwa na Waziri Mkuu Majaliwa

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Kassim Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Kassim

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, anatarajiwa kufanya ziara ya siku tano itakayokwenda sanjari na uzinduzi wa miradi, kukagua na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Charles Mbuge, alisema katika ziara hiyo inayoanza leo, atatembelea miradi hiyo 10 yenye thamani ya Sh bilioni 855.

Kati yake, minane ni ya serikali yenye thamani ya Sh bilioni 845 na miwili ni ya watu binafsi ikiwa na thamani ya Sh bilioni 10. Mbuge alisema miradi hiyo ni ya ujenzi wa maegesho ya magari makubwa Nyakanazi wenye thamani ya Sh bilioni 2.6, Ngara miradi miwili, kiwanda cha kukoboa Kahawa Ngara wenye thaman ya Sh bilioni sita na mradi wa kufua umeme wa maji Rusumo wenye thamani ya Sh bilioni 816.

Miradi mingine iliyopo wilayani Kyerwa ni kiwanda cha kuchenjua madini ya Tini wenye thamani ya Sh bilioni nne , mradi wa jengo la Tanesco wenye thamani ya Sh milioni 483.4 , mradi wa jengo la ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Kyerwa wenye thaman ya Sh milioni 703.3.

Katika Wilaya ya Karagwe, atazindua na kukagua miradi miwili ambayo ujenzi wa hospitali ya wilaya wenye thamani ya Sh bilioni 2.3 na mradi wa Chuo Cha Ufundi Stadi VETA wenye thamani ya Sh bilioni 15.8.

Aidha katika ziara hiyo, waziri mkuu atawasalimia wananchi pamoja na kuhamasisha shughuli za maendelea pamoja na kuwaeleza miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali.