Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 29Article 560302

Uhalifu & Adhabu of Wednesday, 29 September 2021

Chanzo: mwananchidigital

Mke wa mshtakiwa kesi ya kina Mbowe aanza kutoa ushahidi

Mke wa mshtakiwa kesi ya kina Mbowe aanza kutoa ushahidi Mke wa mshtakiwa kesi ya kina Mbowe aanza kutoa ushahidi

Lilian Kibona (25) shahidi wa tatu wa upande wa utetezi katika kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi, inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu ameanza kutoa ushahidi katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.

Kibona ambaye ni mke wa mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo, Adam Kasekwa, ameanza kutoa ushahidi wake leo Jumatano Septemba 29, 2021, mbele ya Jaji Mustapha Siyani.

Shahidi huyo, anaongozwa kutoa ushahidi wake na wakili wa utetezi, John Mallya.