Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 13Article 585571

Habari Kuu of Thursday, 13 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Mkenda kutumia mkakati huu Wizara ya Elimu

Prof. Adolf Mkenda, Waziri wa Elimu Prof. Adolf Mkenda, Waziri wa Elimu

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema atatumia wataalam wa elimu wa ndani na nje ya wizara ili kuwa na maamuzi yenye tija kwa nchi.

Waziri Mkenda amesema hayo leo jijini Dodoma wakati akikabidhiwa ofisi na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Prof. Joyce Ndalichako, ambapo ameongeza kuwa katika uongozi wake hatatoa maamuzi juu ya sekta ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ubunifu bila ya kushauriana na wataalam husika katika sekta hiyo.

Profesa Mkenda amesema anafanya hivyo kwa kuwa Wizara hiyo inahitaji utulivu na siyo ya kubadilisha mambo ama kutoa matamko bila kuzingatia maoni ya wataalam kwani kufanya hivyo ni kuwachanganya wananchi.