Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 29Article 544771

Habari za Mikoani of Tuesday, 29 June 2021

Chanzo: eatv.tv

Mkinga Mkinga azikwa Chato

Mkinga Mkinga azikwa Chato Mkinga Mkinga azikwa Chato

Mwili wa aliyekuwa Mwandishi wa Habari na baadae kuwa Mhariri na Mkurugenzi mwenza wa kampuni ya uchapishaji ya gazeti la Jamhuri, Marehemu Mkinga Babu Mkinga umezikwa kijini kwao Bwina wilayani chato Mkoani Geita.

Submitted by Elbogast on Jumatatu , 28th Jun , 2021Marehemu Mkinga Mkinga amezikwa leo huku mamia ya ndugu, jamaa na marafiki wakielezea pengo aliloliacha na mchango wake katika taaluma yake ya uandishi.

Akimuelezea Marehemu Mkinga, Mwenyekiti wa wazee Chato, Mzee Bigambo Biseko amesema kuwa Mkinga ni mmoja wa tunda la Chato huku akihuzunika kuwa ametangulia mbele za haki ilihali bado walikuwa wanamuhitaji hasa alipojitolea kujenga shule.

Marehemu Mkinga Babu Mkinga alifariki usiku wa kuamkia JuniĀ 24, 2021, katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili MOI, jijini Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa, na marehemu ameacha mke na Mtoto mmoja.