Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 07Article 541486

xxxxxxxxxxx of Monday, 7 June 2021

Chanzo: eatv.tv

Mkufunzi afunguka Mshahara wa Panya Magawa

Mkufunzi wa Panya Magawa Pendo Msegu amesema suala la malipo la Panya huyo ambaye anastaafu mwezi huu wa sita lipo kiutaratibu wa Serikali ya pande mbili kati ya Tanzania na Cambodia.

Submitted by Shaluwa Anta on Jumatatu , 7th Jun , 2021 Picha ya Panya Magawa

"Kuhusu malipo naomba nisilisemee sana kuna ishu za kiutawala na makubaliano maalum kati ya Serikali huku na ya kule na malipo yake yanakuja na kitu anachokifanya, tunaamini kile kinachofanywa atunzwe ndiyo anastahili kukipata ili aweze kutusaidia kutuonesha mabomu na kuokoa maisha ya watu", ameeleza Mkufunzi wa Panya Magawa Pendo Msegu. 

Panya Magawa alipata umaarufu mkubwa hapa nchini Tanzania baada ya kutunukiwa Nishani ya Kimataifa ya Dhahabu kutokana na uwezo wake wa kubaini mabomu ya kutegwa ardhini katika Taifa la Cambodia.

Join our Newsletter