Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 06Article 555571

Habari za Mikoani of Monday, 6 September 2021

Chanzo: Mwananchi

Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Malinyi apata ajali

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi, Joanfaith Kataraiya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi, Joanfaith Kataraiya

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi, Joanfaith Kataraiya na dereva wake wamepata ajali baada ya gari waliyokuwa wakisafiria kupasuka tairi ya mbele na kupinduka katika Kijiji cha Usangule wilayani Malinyi.

Akizungumza Mwananchi kwa njia ya simu Mkuu wa Wilaya hiyo, Mathayo Masele amesema ajali hiyo ilimetokea Septemba 05, mwaka huu saa moja kasoro jioni.

Masele amesema walipata taarifa ya ajali hiyo majira ya jioni kutoka kwa mkurugenzi mwenyewe baada ya kunusurika na walifika eneo la ajali kijiji cha Usangule kilometa 25 kabla ya kufika Malinyi.

Amesema licha ya maendeleo mazuri ya mkurugenzi huyo aliyejeruhiwa zaidi miguuni na dereva aliyelalamikia kuumia mgongo na kichwa, ajali hiyo ilikuwa ni mbaya kwa tairi kupasuka na gari kupinduka na tairi kuwa juu.