Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 23Article 553033

Dini of Monday, 23 August 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Mkurugenzi Tumaini Media kuagwa leo

Mkurugenzi Tumaini Media kuagwa leo Mkurugenzi Tumaini Media kuagwa leo

MWILI wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Tumaini Media, Taasisi ya habari inayomilikiwa na Kanisa Katoliki, Padre Paul Haule unatarajiwa kuagwa leo katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petro, Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Taarifa ya kanisa ilieleza kuwa Padre Haule anaratajiwa kupelekwa kanisani saa 11 na nusu jioni kwa ajili ya misa ya kumuombea na baadaye kutakuwa na mkesha.

Kesho asubuhi mwili unatarajiwa kuondolewa kanisani hapo kupelekwa katika kituo cha hija Pugu nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam kwa maziko.

Katika kituo hicho kutafanyika misa ya mazishi na pia waumini watapata fursa ya kutoa heshima za mwisho.

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) katika salamu za rambirambi lilisema linatambua mchango wa Padre Haule katika uinjilishaji kupi- tia vyombo vya kisasa vya mawasiliano.

Padre Haule aliaga dunia Agosti 18 mwaka huu katika Hospitali ya Kardinali Rugambwa Ukonga, Dar es Salaam