Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 24Article 553405

Uhalifu & Adhabu of Tuesday, 24 August 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Mkurugenzi Wilaya mbaroni kwa wizi wa mabati

Mbaroni kwa wizi wa mabati Mbaroni kwa wizi wa mabati

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linawashikilia watu saba wakiwemo maafisa ugani wa wilaya ya Kilosa pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi wa Wilaya ya hiyo Asajile Mwambambale kwa tuhuma za wizi wa mabati mali ya Halmashauri yenye thamani zaidi ya shilingi milioni 30.

Akitoa taarifa matukio mbalimbali ya kiuhalifu ndani ya mkoa wa Mkoa huo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, SACP, Fortunatus Musilimu, amethibitisha kushikiliwa kwa watuhumiwa hao kwa tuhuma za upotevu wa mabati hayo kwenye stoo ya Halmashauri.

Aidha Kamanda Musimu ametoa angalizo kwa wananchi wa mkoa Morogoro wenye nia za kujihusisha katika uhalifu, kutofanya hivyo kwani jeshi la polisi limejipanga vyema katika kuhakikisha usalama wa raia na mali za umma zinalindwa na wahalifu hawatofanikiwa kutokana na oparesheni za jeshi hilo.