Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 10Article 584686

Habari Kuu of Monday, 10 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Mkuu wa Jeshi la Wanamaji Tanzania azungumza na Mkuu wa Jeshi Pakistan

Mkuu wa Jeshi la Wanamaji Tanzania akutana na Mkuu wa Jeshi Pakistan Mkuu wa Jeshi la Wanamaji Tanzania akutana na Mkuu wa Jeshi Pakistan

Kamanda wa Jeshi la Wanamaji wa Tanzania, Michael Mwandenje Mumanga amefanya ziara ya kikazi nchini Pakstan ambako alikwenda kwa mwaliko wa Mkuu wa Majeshi Muhammad Amjad Khan Niazi.

Kamanda Michael ametembelea Makao Makuu ya Jeshi la Wanamaji nchini Pakistan na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Majeshi wa Pakistan, Muhammad Amjad Khan Niazi.

Wakuu hao wametoa maoni yao kuhusu masuala ya maslahi ya pande zote mbili na ushirikiano wa nchi mbili kwa ajili ya Usalama wa baharini na amani.

Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Tanzania Admirali Michael Mwanandenje Mumanga amepongeza jukumu la Pak Navy katika usalama wa baharini katika eneo hilo.

Mwanandenje Mumanga ameyasema hayo wakati akizungumza na Mkuu wa Wanajeshi Admiral Muhammad Amjad Khan Niazi huko Islamabad tarehe 10 Januari.

Baada ya kuwasili kwa Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Tanzania Micharl Mwanandenje Mumanga katika makao makuu ya jeshi la wanamaji la Pakistani huko Islambad, kamanda huyo alikaribishwa kwa moyo mkunjufu na Jeshi la Wanamaji la Pakistani na kumkabidhi ulinzi wa kitamaduni wa heshima.

Wakuu wa wanamaji wa Jeshi la Wanamaji la Tanzania na Jeshi la Wanamaji la Pakistan walijadili mambo rasmi yanayohusiana na kukuza ushirikiano wa pande zote na wa nchi mbili za baharini.

Msemaji wa Jeshi la Wanamaji la Pakistan pia alisema kuwa:

Ziara ya Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Tanzania itasaidia kuimarisha zaidi uhusiano kati ya nchi hizo mbili, Pakistan na Tanzania.