Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 28Article 554134

Habari za Mikoani of Saturday, 28 August 2021

Chanzo: ippmedia.com

Mkuu wa Shule aonywa kwa kumkaribisha Amber Rutty kuwa mgeni rasmi

Mkuu wa Shule aonywa kwa kumkaribisha Amber Rutty kuwa mgeni rasmi Mkuu wa Shule aonywa kwa kumkaribisha Amber Rutty kuwa mgeni rasmi

UONGOZI wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke umeonesha kuchukizwa na kitendo cha Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nzasa cha kumualika Amber Rutty kuwa kama mgeni rasmi na kuongea na Wanafunzi.

“Kumekua na taarifa zinazosambaa kupitia kipande cha video mitandaoni zikimuonesha mtu mmoja akitembelea Shule ya Msingi Nzasa iliyopo Temeke, akiwa amevaa mavazi yaliyo kinyume na maadili ya Kitanzania”

“Tunapenda kutoa taarifa kwamba uongozi wa Manispaa ya Temeke umechukizwa na ugeni huo, umemuonya Mkuu wa Shule kwa kukiuka maadili ya utumishi wa umma kutokana na kitendo kilichotokea na Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza” kimesema Kitengo cha Habari na Uhusiano, Manispaa ya Temeke.