Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 23Article 559333

Habari za Mikoani of Thursday, 23 September 2021

Chanzo: millardayo.com

Mlemavu aliepewa pesa ya Bajaji na hayati Magufuli aibiwa bajaji (video+)

Mlemavu aliepewa pesa ya Bajaji na hayati Magufuli aibiwa bajaji (video+) play videoMlemavu aliepewa pesa ya Bajaji na hayati Magufuli aibiwa bajaji (video+)

Nyangoma James ni Mlemavu ambaye Hayati Magufuli alimchangia Mil 5 Ubungo Dar es salaam na akachangisha Watu wengine hadi ikapatikana zaidi ya Tsh. Milion 8 ambayo Nyangoma alinunua Bajaji na akawa Dereva yeye mwenyewe akiwa anafanyia biashara, lakini Jumamosi Wiki hii Bajaji yake imeibwa nyumbani alikopanga Kibaha, Mkoani Pwani.

Licha ya kuwa na Watoto watatu ambao wawili anawasomesha kwa sasa, Nyangoma pia anaishi na Baba yake Mzazi ambaye amepooza miguu na ile Bajaji aliyoinunua kwa msaada wa Hayati Magufuli ndio ilimwezesha kuwahudumia Watoto na Baba yake, namba za kumsaidia 0758311341 (imesajiliwa kwa jina la Joyce Songora).