Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 03Article 540691

Habari za Mikoani of Thursday, 3 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Mongela ataka umakini miradi ya maendeleo

MKUU wa Mkoa wa Arusha, John Mongela, amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, Waziri Morice, kusimamia miradi ya maendeleo na mapato ili kusiwe na hoja kwenye ukaguzi wa hesabu za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Aidha, ametoa rai kwa vyombo vya ulinzi na usalama kuwa timamu na kutovumilia tishio lolote litakalovunja amani.

Mongela aliyasema hayo jana wilayani Karatu wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri hiyo katika ziara yake kujitambulisha na kukagua miradi itakayozinduliwa na Mwenge wa Uhuru utakaoingia mkoani Arusha Juni 16, mwaka huu na kukimbizwa katika halmashauri saba za mkoa huo.

Alimsisitiza mkurugenzi huyo kusimamia vema mapato, matumizi na miradi mbalimbali ili kuondoa maswali yanayoulizwa na wakaguzi wakati wa ukaguzi wa miradi na shughuli mbalimbali za kimaendeleo.

"Mimi sijui kila kitu na hakuna mtu anajua kila jambo, lazima umsikilize kila mtu usidharau hoja zao kisha, yapime kabla ya kuchukua hatua na sitavumilia mtu atakayesababisha nichukue maamuzi yanayostahili kuchukuliwa, naomba tuwe kitu kimoja tushirikiane ili tuujenge mkoa wetu," alisema.

Michezo

Biashara

Burudani

Afrika

Maoni