Uko hapa: NyumbaniHabari2021 05 27Article 540130

Uhalifu & Adhabu ya

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Morogoro: Mbaroni kwa Kufukua Maiti na Kunyofoa Viungo

Morogoro: Mbaroni kwa Kufukua Maiti na Kunyofoa Viungo Morogoro: Mbaroni kwa Kufukua Maiti na Kunyofoa Viungo

Watu watatu wanashikiliwa na Polisi mkoani Morogoro kwa tuhuma za kufukua mwili wa Rehema Michel, aliyezikwa Jumapili na kutoa viungo mbalimbali ikiwamo kichwa, figo na sehemu za siri.

Mwili wa marehemu Rehema ulizikwa kwenye makaburi ya familia katika Kijiji cha Nguyami, Kata ya Idibo wilayani Gairo mkoani Morogoro.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Fotunatus Musilimu alisema tukio hilo lilitokea jana alfajiri katika eneo ambalo ni umbali wa mita 50 kutoka kwenye makazi ya watu kijijini hapo.

Musilimu alisema taarifa za awali zilieleza kwamba mwanamke huyo (35) alipata ajali mjini Morogoro na kulazwa katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro na siku chake baadaye alifariki dunia.

Alisema mwili wa mwanamke huyo ulihifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti hospitalini hapo na Mei 23, 2021 (Jumapili) ulisafirishwa na kuzikwa siku hiyo. “Baada ya kumaliza mazishi, leo alfajiri (juzi) kulipokucha wakakuta kaburi limefukuliwa na mwili umetolewa kwenye sanduku.

Mwili ulikutwa umekatwa badhi ya viungo ambavyo ni kichwa, sehemu za siri, shingo, mkono na mguu wa kushoto na kuupasua mwili na kuchukua pafu la kushoto na moyo,” alisema.

Join our Newsletter