Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 14Article 557326

Habari za Mikoani of Tuesday, 14 September 2021

Chanzo: Jamii Forums

Morogoro: Watoto zaidi ya 1200 wapata ujauzito ndani ya mwaka mmoja

Mimba za Utotoni Mimba za Utotoni

Matukio ya Mimba na NdoaZaUtotoni yamezidi kuongezeka katika Mkoa wa Morogoro, ikielezwa ndani ya kipindi cha mwaka mmoja (2020/21) Watoto wapatao 1,277 wamepata Ujauzito.

Afisa Ustawi wa Jamii Mkoani humo, Jesca Kamugela amesema Halmashauri zote za Morogoro zimekuwa zikiripoti matukio hayo na mmomonyoko wa maadili umetajwa kuwa chanzo

Hata hivyo, kumekuwa na changamoto kubwa sana kwenye maswala ya ulezi, wazazi wengi mikoani hasa vijijini wanawachia watoto kulelewa na bibi na babu uwangalizi unakuwa mdogo hii pia ni chagamoto kubwa kupelekea watoto kujingiza kwenye makundi na kupata vishawishi

Kwa mujibu wa takwimu za 2020 za Shirika la Afya Duniani (WHO), kila mwaka katika maeneo yanayoendelea Wasichana wapatao Milioni 21 wenye umri kati ya miaka 15-19 hupata Ujauzito.