Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 09Article 584440

Habari Kuu of Sunday, 9 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Moshi kufanya haya miaka 45 ya CCM

Moshi kufanya haya miaka 45 ya CCM Moshi kufanya haya miaka 45 ya CCM

Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Moshi Mjini mkoani Kilimanjaro kimesema kitatumia wiki ya maadhimisho ya miaka 45 tangu kuzaliwa kwa chama hicho kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kupata chanjo ya Uviko-19 na uchangiaji wa damu salama.

Hayo yamebainishwa na katibu wa CCM Wilaya hiyo, Ibrahim Mjanakheri wakati akizungumza maandaliziya maadhimisho hayo, ambapo amesema kwa Moshi wataanza kuadhimisha Januari 26 na kilele ni Februari 5, 2022.

"Februari 5 ya kila mwaka tunaadhimisha kuzaliwa kwa chama chetu, mwaka huu tunatimiza miaka 45 na tutaanza maadhimisho haya Januari 26 ambapo kila siku tutakuwa na kitu cha kufanya katika kuwaweka wananchi pamoja na kuimarisha chama".

"Moja ya shughuli tutakazozifanya ni kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kupata chanjo ya Uviko-19 kama ambavyo Serikali imekuwa ikielekeza, na tayari tumeongea na mganga mkuu wa Mkoa ili kulifanya hili" amesema.

Ameongeza kuwa "Pia tumepanga kuchangia damu salama na kuhamasisha wananchi kujitokeza kuchangia damu ili kusaidia kuokoa maisha ya watu mbalimbali wenye uhitaji wa damu".

Mjanakheri amesema katika wiki hiyo ya maadhimisho wataweka msukumo katika uandikishaji wanachama wapya na kuwasajili katika mfumo wa kielektroniki.