Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 20Article 573004

Habari Kuu of Saturday, 20 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Moto Wateketeza Maduka Bunju B

Moto Wateketeza Maduka Bunju B Moto Wateketeza Maduka Bunju B

Moto mkubwa umeteketeza maduka kadhaa ya wafanyabiashara katika eneo la Bunju 'B' wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam na kusababisha wafanyabiashara hao kupoteza mali zao zilizokuwemo ndani ya maduka yao na wasijue nini cha kufanya.

Baadhi ya mashuhuda katika eneo hilo wamedai chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme katika moja ya maduka hayo lililokuwa likihifadhi mabetri ya gari, na kwamba moto huo umeanza majira ya alfajiri.

Hadi sasa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji kinaendelea na zoezi la kuuzima moto huo ambao bado unaendelea kuwaka katika baadhi ya maduka.