Uko hapa: NyumbaniHabari2021 08 20Article 552745

Habari za Mikoani of Friday, 20 August 2021

Chanzo: MWANANCHI

Moto waua wawili familia moja

Watoto wawili wafariki kwa ajali ya moto Watoto wawili wafariki kwa ajali ya moto

Watoto wawili wa familia moja wakazi wa Tarakea wilayani Rombo wamefariki baada ya nyumba yao waliyokuwa wakiishi kuungua kwa moto.

Akitoa taarifa hiyo leo Ijumaa Agosti 20, 2021 Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Hamis Maiga ameeleza tukio hilo limetokea jana usiku uliosababishwa na mshumaa.

Hamisi amesema watoto ambaye mmoja ana miaka sita, na mwingine ana mwaka mmoja

"Mwanamke mmoja mwenye watoto wawili aliwasha mshumaa baada ya luku yao kwisha, baada ya kuwasha mshumaa akawa ametoka nje kidogo.

“Mshumaa alikuwa ameweka kwenye meza ya plastiki ndipo mshumaa ulipodondokea kwenye meza na kushika kwenye mabanzi ambayo yalishika moto na nyumba yote yenye vyumba 10 kuteketea," amesema Maiga.

Maiga amesema kwa sasa Kamati ya Ulinzi ya wilaya hiyo inaelekea kwenye eneo la tukio.