Uko hapa: NyumbaniHabari2021 06 06Article 541243

Habari Kuu of Sunday, 6 June 2021

Chanzo: www.habarileo.co.tz

Mpango ataka wahalifu wa mazingira wabanwe

Mpango ataka wahalifu wa mazingira wabanwe Mpango ataka wahalifu wa mazingira wabanwe

MAKAMU wa Rais, Dk Philip Mpango amesema Serikali ya Awamu ya Sita haitavumilia kuona uharibifu wa mazingira ukiendelea, akisistiza wahalifu wote katika eneo hilo watachukuliwa hatua kali.

Aidha, amewaambia wakuu wa mikoa na makatibu tawala wao kwamba watapimwa utendaji wao kutokana na utekelezaji wa agizo la kila halmashauri kupanda miti milioni 1.5.

Alitoa maagizo hayo jana katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani iliyokwenda sambamba na uzinduzi wa kampeni ya mazingira, jijini Dodoma.

“Vitendo vya uharibifu wa mazingira ni dhuluma na ukatili kwa vizazi vijavyo na kwa jamii ya watanzania kwa ujumla. Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, haitavumilia kuona dhuluma hiyo ikiendelea… tutahakikisha wahalifu wote wa mazingira wanachukuliwa hatua kali za kisheria,” alisema.

Alisisitiza, “ Binaadamu tunategemea kupata chakula na hewa safi kutoka kwenye mimea, mimea nayo inategemea hewa ukaa kutoka kwa binadamu na wanyama, lakini pia wote tunahitaji ardhi na maji kuweza kuishi.”

Alisema Tanzania kama zilivyo nchi nyingine zinategemea kwa kiasi kubwa kuni na mkaa kwa ajili ya kupikia na kusisitiza haja ya kutumia nishati mbadala ili kukabiliana na uharibifu huo.

Dk Mpango alisema tathimini iliyofanyika kupitia utafiti wa mapato na matumizi ya kaya binafsi 2017/18, zinaonesha kila kaya 100 nchini, kaya 90 zinatumia kuni na mkaa kama nishati ya kupikia.

“ Takwimu zinaonesha kuwa asilimia 80 ya uharibifu wa rasilimali za misitu katika maeneo mengi nchini inatokana na matumizi ya nishati ya kuni na mkaa na yanaongezeka hata Mijini kwenye nishati ya umeme.”

“ Takwimu zinaonesha kuwa asilimia 80 ya uharibifu wa rasilimali za misitu katika maeneo mengi nchini inatokana na matumizi ya nishati ya kuni na mkaa na yanaongezeka hata Mijini kwenye nishati ya umeme.”

sawa na tani 45,000 za mkaa, sawa na mita za ujazo 75,000 za miti na sawa na ekari 188 za miti zinazokatwa kwa mwaka.

Dk Mpango alisema nchi inaweza kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa kwa kutumia nishati mbadala kama mafuta ya kaa, gesi, umeme,bayogesi, nishati ya jua pamoja na vitofali vya mkaa wa kupikia.

Alitoa mwito kwa wafanyabiashara wa gesi ya kupikia kubuni mbinu kusaidia wananchi wa kipato cha chini waweze kumudu gharama ya nishati mbadala.

“ Hivyo nisisitize mamlaka husika ikiwemo tamisemi, ofisi ya makau wa rais, maliasili na utalii, nishati, TFS na wadua wa maendeleo kubuni na kuteleza mikakati ya kuongeza utumiaji wa nishati mbadala kwa gharama nafuu,” alisema.

Jafo, ma RC watwishwa mzigo Akizungumzia kampeni kabambe ya usafi na uhifadhi wa Mazingira, Dk Mpango alimuagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Selemani Jafo (pichani) kuisimamia siku kwa siku na kuhakikisha inafanikiwa.

“ Kampeni umeianzisha mwenyewe na utapimwa na mafanikio ya hiyo kampeni. Ile miti iliyopandwa siku ya matembezi uhakikishe haifi na mimi nitaikagua,” alisema.

Alitoa maagizo kadhaa kwa watendaji wote wa wizara, wakuu wa Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa na wadau ikiwamo kuwataka wahamasishe wananchi juu ya utunzajia mazingira, kufuatilia utekelezaji na kutolea taarifa. Juhudi hizo zinajumuisha upandaji miti ya biashara, matunda na dawa na kila kaya ikapanda miti.

Alielekeza halmashauri zote kusimamia na kudhibiti uharibu mazingira kwa sababu ya wivu, uonevu au imani potofu, wafungaji kuchunga ndani ya mashamba ya mazao ya miti na kukata miti kwenye hifadhi kwa kuiba.

Alikumbusha kila mkuu wa mkoa na katibu Tawala wake kutimiza lengo la kupanda na kutunza miti isiyopungua milioni 1.5 katika hamshauri zao. “ Na hili nawakumbusha na tutakaguana sana na litakuwa miongoni mwa mambo ambayo tutawapima utendaji wenu,” alisema.

Alizitaka halmashauri na TFS kuongeza jitihada kusimamia mapori na rasilimali, kuzuia moto na kupanga matumizi ya misitu yaweze kuwanufaisha watanzania Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Jafo, alisema maadhimisho ya wiki ya mazingira Tanzania yalifanyika kwa mafanikio katika upandaji miti, maonesho kuhusu nishati mbadala na mafunzo kwa maofisa mazingira ngazi ya serikali za mitaa na serikali kuu.

Alisema pia, nchi itazindua kampeni kabambe ya utunzaji mazingira kwa lengo la kuhamasisha utunzaji na uhifadhi mazingira nchini katika maeneo mbalimbali

nchini.

Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya Uratibu wa Kampeni ya Mazingira Nchini, Seif Ali Seif, alisema mabadiliko ya mazingira yamesababisha vipindi vya mvua na kiangazi kushindwa kutabirika kama zamani.

Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira, (UNEP) Clara Makenya, alisema shirika hilo litaendelea kuwa mdau wa mstari wa mbele kuwezesha shughuli za utunzaji mazingira nchini.

Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Zlatan Milizic, alisema Siku ya Mazingira Duniani ilianzishwa kwa madhumuni ya kuwakutanisha wadau wa mazingira kujadili namna bora ya kuhifadhi mazingira kwa lengo la kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Mazingira, Viwanda na Biashara, David Mwakiposa, alipongeza juhudi za serikali katika kutunza mazingira.

“Kamati inashauri serikali ikaangalia matumizi ya nishati ya mkaa, kwa sababu Dar es Salaam licha ya wakazi wake kutumia nishati ya umeme kwa asilimia 90, lakini matumizi ya mkaa yanazidi asilimia 70,” alibainisha.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Antony Mtaka, alisema atahakikisha utunzaji mazingira unakuwa kipaumbele kama ambavyo serikali imekuwa ikisisitiza.

Join our Newsletter