Uko hapa: NyumbaniHabari2021 11 18Article 572347

Habari za Afya of Thursday, 18 November 2021

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Mpango jumuishi wa lishe watekelezwa kwa 80%

Jenista Muhagama, Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana na  Walemavu Jenista Muhagama, Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Walemavu

Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu Sera, bunge, kazi, ajira, vijana na wenye ulemavu Jenista Mhagama amewataka watendaji wanaohusika na afua za lishe nchini kusimamia vema taratibu za upatikanaji na ulaji wa lishe bora ili kujenga taifa imara na lenye nguvu.

Waziri Jenista ametoa kauli hiyo jijini Tanga wakati alipokua akitoa taarifa ya mpango jumuishi wa kwanza wa lishe ulioanza rasmi nchini kwenye mwaka wa fedha 2014/ 2015.

Amesema swala la lishe ni swala linalotakiwa kupewa kipaumbele kuanzia ngazi ya familia mpaka taifa lengo likiwa ni kutoa makuzi bora ili kuepuka udumavu.