Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 20Article 558631

Siasa of Monday, 20 September 2021

Chanzo: TanzaniaWeb

Msajili kukutana na polisi Septemba 23

Jaji Francis Mutungi, Msajili  wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi, Msajili wa Vyama vya Siasa

Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi amesema Septemba 23 , atafanya kikao na Jeshi la Polisi mjini Dodoma huku lengo la kikao hicho likiwa ni kuhakikisha wanafanya majadiliano kabla ya kukutana na wadau.

Jaji Mutungi, amesema kuwa baada ya kikao hicho, ndipo watakutana na Kamati ya uongozi wa baraza la wanasiasa tarehe 30 mwezi Septemba ili kupokea maoni ya upande wao.

"Tarehe 23 mwezi tisa, nitafanya kikao na Jeshi la polisi dodoma, ili tutakapokutana na wadau tuwe na data za kweli zilizofaniwa kazi sio za kumbumba" Jaji Mutungi

Ofisi ya Msajili wa Vyama ilitangaza kukutanana vyama vya siasa, pamoja na Jeshi la Polisi ili kujadili tofauti zilizopo baina yao kwa ajili ya kupata utatuzi wa kudumu kwa kile kilichodaiwa kuwa sintofahamu iliyo baina ya pande hizo mbili kuchafua taswira ya nchi .