Uko hapa: NyumbaniHabari2021 09 23Article 559345

Habari Kuu of Thursday, 23 September 2021

Chanzo: globalpublishers.co.tz

Msajili wa Vyama Akutana na Timu ya IGP Sirro

Msajili wa Vyama Akutana na Timu ya IGP Sirro Msajili wa Vyama Akutana na Timu ya IGP Sirro

Msajili wa vyama vya siasa, Jaji Francis Mutungi leo amekutana na maafisa wakuu waandamizi wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dodoma, akiwemo IGP Simon Sirro ikiwa ni maandalizi ya kikao kati ya wadau wa siasa, msajili na polisi kitakachofanyika Oktoba 21, 2021.Mnamo Septemba 6, 2021, Jaji Mutungi aliwaambia waandishi wa habari jijini Dodoma kuwa ofisi yake kwa kushirikiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi imepanga kukutana na wadau wa siasa kufuatia malalamiko ya kutopewa fursa ya kufanya kazi zao za siasa kwa kuzuia kufanya makongamano mbalimbali.