Uko hapa: NyumbaniHabari2022 01 15Article 586054

Siasa of Saturday, 15 January 2022

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Msama ajitokeza kuchukua fomu ya Uspika

Msama ajitokeza kuchukua fomu ya Uspika Msama ajitokeza kuchukua fomu ya Uspika

Mfanyabiashara Maarufu nchini, Alex Msama ameungana na makada wengine wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kujitokeza kuchukua fomu kwa ajili ya kigombea nafasi ya kiti cha Spika ambayo imeachwa wazi baada ya aliyekuwa Spika Job Ndugai kujiuzulu.

Msama anajitokeza kuchukua na kisha kuirudisha fomu hiyo leo Jumamosi Januari 15,2021 katika ofisi ndogo za CCM Lumumba, saa chache kabla ya kufungwa kwa shughuli hiyo alisema nia yake ni kuliongoza Bunge hilo ambalo ni moja kati ya mihimili mitatu ya nchi.

Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu hiyo, Msama alisema amejitokeza kuomba ridhaa ya kuteuliwa na chama chake kugombea Uspika kutokana na kukidhi matakwa ya kikatiba kugombea nafasi hiyo adhimu katika Taifa.

"Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa afya njema na kuweza kuamka kukamilisha hatua hii ya uchukuaji fomu kuomba nafasi katika chama changu, hii no nafasi kipekee na historia kubwa katika maisha yangu, na ninajiamini uwezo ninao kwani mbali na kumtegemea Mungu kwa kwa kuwa yeye ndio muweza wa yote pia ninaweza, hivyo nitaijaza fomu hii leoleo na kuirudisha "alisema Msama

Uchukuaji fomu ulianza Januari 10 baada ya kutangazwa nafasi ya uspika kuwa wazi kutokana na kujiuzulu kwa aliyekuwa Spika wa Bunge hilo,Job Ndugai Januari 6,2022.

Aidha kwa mujibu wa Msaidizi Mkuu idara ya Oganaizesheni Solomon Itunda, hadi kufika jana wanachama 66 wamehitokeza kuchukua fomu kuomba kuwania kiti hicho.